Alhamisi, 21 Aprili 2016

VIJUE VITU VINNE MUHIMU KATIKA KUPAMBA NYUMBA TANZANIA

Katika Tanzania nyumba ni sehemu ya muhimu sana muda mwingi hutukuta katika nyumba zetu wageni rafiki zetu hutembelea nyumba zetu.Tungependa sana kuona nyumba zinapendeza zinavutia.Hapa unaweza kujionea namna utapamba nyumba yako na kuifanya iwe ya kuvutia sana kwa kuzingatia mambo yafuatayo manne.
 
Ujumbe
 
Hii ni hatua ya kwanza ya upambaji.lazima uzingatie ujumbe unaotaka kuufikisha kwa jamii unapotaka kupamba nyumba yako.Unaweza kutoa ujumbe wa tamaduni ulionayo hususani kabila,nchi na kupata mapambo ya nyuma yako.Unaweza ukaangalia daraja unalotaka nyumba yako ionakane ya daraja la utajiri,maskini au la kati.pia unaweza ukapamba jinsi ulivyo mfano vitu vya jinsia yako.
Rangi
 
Hii ni hatua ya pili ya upambaji ambapo baada ya ujumbe kujulikana rangi zitaendana sambamba na ujumbe unaotaka kuutoa na kupendezesha nyumba yako zaidi.Pia rangi ukiziweka sehemu mbalimbali kama samani za ndani,madirisha,na vifaa mbalimbal vya ndani.vitapendezesha nyumba yako zaiadi ya kuweka Randi kwenye ukuta tu.
 
nafasi
matumizi ya nafasi kama kuweka vitanda vyenye makabati,makichi ya vitanada,vitanda vya makiochi,vinasaidia sana kutunza nafasi na kuacha chumba chako kikiwa kimependeza sana.
 
vitu vya kumbukumbu
unaweza ukatumia meza za zamani ,viti vya zamani,ukaviboresha  na kuonekana muonekano mzuri pasipo kuviuza au kuvitupa
HII NI LINK YA NYUMBA YAKO KUELEZEA ZAIDI VITU VINEE YA KUPAMBA NYUMBA..
http://ghar360.com/blogs/home-decor/4-key-aspects-of-home-decoration-to-consider
SEBULE IKIWA IMEUNGANISHWA NA CHUMBA CHA KULIA CHAKULA
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
RANGI YA MAKOCHI IKIWA IMEFANANISHWA NA RANGI YA UKUTA.

Ijumaa, 15 Aprili 2016

KUPAMBA NYUMBA KWA SAA HUFANYA NYUMBA YAKO ITAMBULIWE PIA IWE YA KISASA

Katika nyumba nyingi hapa kwetu Tanzania  kupamba nyumba kwa saa imeonekana ni suala la  kawaida na lisilona maana yeyote.
kupamba kwa nyumba kwa saa kutapendesha nyumba yako.

Unapofanya saa kuwa urembo wa nyumba yako yafuatayo ni ya kuzingatia:

  • Chagua saa yenye umbo la mstatili kwa kuweka chumbani ili
chumba kionekane kilichotulia.

  • Chagua saa yenye umbo la urembo lililochongwachongwa kwa ajili ya kuweka sebileni ili lipendezeshe sebule

  • Chagua saa yenye umbo la duara kwa ajili ya ofisi duara ni nene itafanya bishara yako ionekane inakuwa na ni tajiri.
  • Usiweke saa mahali pa juu sana hivyo kupata shida kuiangalia weka saa katika upeo wa macho iwe rahisi kuifuatilia.


Picha inayaonyesha chumba cha kulia chakula kimepambwa na saa.




Picha kinachoonyesha chumba cha sebule kikiwa kimepambwa na saa.


Hiki ni kiungo cha mtandao kitakachoweza kukuhabarisha zaidi kuhusu saa na upambaji wa nyumba.

http://www.fstips.com/home-feng-shui/29.html
 








 

Jumatano, 13 Aprili 2016

SHERIA,NAFASI NA HAKI YA MAAMUZI KWA MWANAMKE IKIPEWA KIPAUMBELE INAWEZA KUBORESHA NYUMBA YAKO


MWANAMKE
  • Mwanamke ni  wa muhimu sana katika jamii.Mwanamke anahitaji kuthamini katika jamii na si kunyamazishwa kimya,kunyimwa maamuzi sahihi kwa kutumia rushwa na hongo mbalimbali .

  • Zipo haki na sheria mbalimbali za   ambazo zinahitajika apewe mwanamke ili aweze kuleta manufaa.mwanamke anatakiwa apewe haki ya kufanya maamuzi pia maamuzi yake kukubalika.

  • Kwenye urembo wa nyumba mwanamke anaaminika kwa kuimudu nyumba vizuri na kufanya ivutie wakati wote ikilinganishwa na  mwanaume.

  • Mwanamke hana budi kushirikishwa kuchagua rangi ya nyumba,aina ya sakafu ya nyumba,mpangilio wa vyumba katika nyumba ,namna mbali mbali za uwekaji wa mapambo katika nyumba,aina za makochi,meza,kabati anazohitaji.mwananke hapaswi kugandamizwa kabisa kwa kuonekana ndio mchafuzi wa nyumba.

  • Mwanaume hapaswi kupanga,kusafisha nyumba peke yake bila kumshirikisha  mwanamke kwan mwanamke ni mwalimu na rafiki zaidi wa watoto.kumpa nafasi na maamuzi ya mwanamke juu ya kupamba nyumba kutaelimisha watoto kwanba kupamba nyumba ni moja ya desturi nzuri

LINK.
http://organizedhome.com/seasonal-spin/five-tips-spring-cleaning-with-kids?utm_campaign=shareaholic&utm_medium=facebook&utm_source=socialnetwork
MWANAMKE NA MTOTO WAKE KWA AJILI YA USAFI
 
 
 
 
 
 
 

                          VIFAA VYA KUOGEA

Jumamosi, 9 Aprili 2016

JE WAJUA MADIRISHA YANAYOONGEZA USALAMA KATIKA NYUMBA YAKO LINAPOTOKEA JANGA LA MOTO?

HISTORIA  YA JANGA LA MOTO

Katika majiji mengi hasa jiji la Dar es salaam,  kuna familia nyingi zimepoteza wapendwa wao kutokana na janga la moto.

Majanga yanapotokea  kwa kuwa nyumba  za mjini zimejengwa kwa uimara mkubwa,zenye mageti na makufuli mengi .Milango na madirisha yenye vyuma ili kuzuia uhalifu inakuwa ni vigumu sana kuwaokoa watu wakati wa moto.Magari ya kuzima moto huwa yapo mbali na si rahisi kufika kwa wakati.

MOTO MBAYA SANA UNATEKETEZA MALI ZOTE













JANGA LA MOTO NA SABABU ZAKE
Janga la moto hutokea pale moto unapokuwa mkubwa na kusababisha madhara.Sababu za janga la moto .janga  la moto husababishwa na hitilafu za umeme ,hitilafu kwenye majiko ya gesi,mishumaaKatika majiji mengi hasa jiji la Dar es salaam,  kuna familia nyingi zimepoteza wapendwa wao kutokana na janga la moto
 NYUMBA IKITEKETEA MOTO BILA HURUMA




MADIRISHA YA USALAMA

MADIRISHA ya usalama ni madirisha yenye uwazi maalum yaliyowekwa  ajili ya kutorokea au kuokolea wakati wa ajali za moto au majanga mengine .Madirisha ya usalama hutumia wavu laini uliorahisi kutoboka ,vioo laini visivyo umiza .dirisha la chuma lililotengenezwa rasmi na kuachwa nafasi maalum wakati wa janga la moto liwe rahisi  kufunguka kwa usalama zaidi. Dirisha hili si mahali pa kuchezea watoto weka kitasa maalum ambapo kitavunjwa baada tu ya ajali ya moto.Usiweke tthamani au kuruhusu watoto kucheza kwenye dirisha.Hakikisha unaweka vibandiko  juu ya dirisha ili kujilisha wageni hilo ni dirisha la usalama.

DIRISHA LA USALAMA LIKIWA LIMEWEKWA ALAMA MAALUM
 
LINK 
HII NI LINK ITAKAYOKUFANYA UWELEWE ZAIDI NAMNA AMBAVYO MADIRISHA YANAONGEZA USALAMA.