Jumanne, 29 Machi 2016

USAFI WENYE KULETA UNGAAVU WA NYUMBA NDIO MPANGO MZIMA.



USAFI
  • Katika maisha usifanye usafi bora liende,utaharibu thamani zako kwa muda mfupi sana utaichukia nyumba  kwani itakuwa chafu muda wote .Asikwmbie mtu nyumba usafi bwana  lazima kuutumikia na kuuheshimu hata kwenye nyumba kwani ndio utakufanya uonekane bomba.  Hata iweje ukinunua viti vyako vipya,meza zako mpya,muhimu kufanyia usafi ukitumia maji na sabuni.
  • Chagua sabuni yenye kuondoa uchafu wa mafuta pia madoa ili kuhakikisha nyumba yako nzima inang'aa.unapoitunia sabuni usiibanie weka kiasi cha kutosha ili kuhakikisha thamani zako pia ukuta,madirisha yanang'aa.tumia maji cha kutosha pia chagua chombo maalum cha kufanyia usafi,dodoki maalum la kufanyia usafi ili ufanye usafi wako kwa uhuru.usiogope kufanya usafi au kushika maji kwani ni namna pekee zitaweza kufanya thamani zako,ukuta,sakafu,vitakate.tumia vifaa vizito yaan vitambaa vyenye kotoni nzito,brashi zenve nyuzinyuzi nzito japo utachoka sana ila mwisho nyumba yako itatakata sana na kuwa mpya.
  • Badilisha ndoo,vitambaa na vifaa vingine pingi vitakapo choka.fanya usafi ukitumia nguvu zako zote kusugua ili patakate,fanya usafi uliomakini angalau mara moja kila siku ili kuhakikisha nyumba yako inakuwa safi wakati wote.kumbuka maji na sabuni hutakatisha nyumba wala hayezeeshi nyumba.pia sehemu za uvunguni nyuma ya milango,nyuma ya makochi usizisahau.
 
 
                                    NYUMBA SAFI IKIWA IMEPAMBWA NA UA

VITI VYA MEZA VIKIWA NA MPANGILIO MZURI 
 
 
 
Mpangilo
  • Jaribu kupanga nyumba na vitu vilivyomo vizuri hakikisha kila kitu kinakaa mahali pake wakati wote hakikisha iwe ni watoto unawaelekeza namna ya kurudishia vitu mahali wanavyovitoa iwe ni sebuleni au mahali popote.

  • Watoto wa umri wowote ni wa kutumia vizuri hasa linapokuja suala la upangaji nyumba hakikisha unawaelekeza kwa upole na wapende kupanga nyumba.nyumba iliyopangwa vizuri ni rahisi sana kuifanyia usafi .ni ngumu sana kukuta panya ,nyoka na wadudu mbalimbali indapo utakuwa makini na haya.

Hitimisho

Usafi huleta raha na mpangilio wa nyumba huleta raha jaribu kusoma na kutenda haya utaona mabadiliko.ukipata mafanikio katika haya usiache kutupatia maoni yako.
LINK

Pia kukitaka kuelewa mbinu zaidi soma stori hii iliyo kwa lugha ya kiingereza
.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni